The House of Favourite Newspapers

Kiungo Mghana Atakayeziba ‘Pengo’ la Mkude Alitua Jana, Kumalizana na Simba Leo

kotei

DAR ES SALAAM: Kiungo ambaye ni raia wa Ghana anayeaminika kuwa amekuja atajiunga na Klabu ya Simba yenye makao yake makuu kunako Mtaa wa Msimbazi jijini Dar, kuziba nafasi ya Jonas Mkude, ametua jana Desemba 7, 2016 hapa nchini akitokea nyumbani kwao.

James Kotei alitua hapa nchini jana jioni majira ya saa 10:50 akitokea kwao Ghana tayari kumalizana na Klabu ya Simba ili ajiunge nayo na kuanza kuitumikia ikiwa ni ingwe ya pili ya Ligi Kuu ya Tanzania, Vodacom Premier League (VPL).

Mchezaji huyo kinda, anasifika zaidi kwa ukabaji na utoaji wa pasi ndefu anatarajia kumalizana na kusaini mkataba na Simba, kesho kwa kuwa mazungumzo ya awali yalishakamilika.

Mratibu wa Simba, Abbas Ally ‘Dizzo’ ndiye aliyejitokeza kumpokea kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na kusema kwamba, baada ya mazungumzo ya mwisho kati yake na klabu hiyo kongwe, taarifa itatolewa.

Tayari Simba wameshamsajilikipa ambaye ni raia wa Ghana kwenye dirisha dogo la usajili ambalo litaisha mwezi huu.

halotel-strip-1-1

MZEE WA MIAKA 76 ALEYETANAGAZA KUTAFUTA MKE “FULL EXLUSIVE INTERVIEW”

Comments are closed.