The House of Favourite Newspapers

Kiungo Yanga Apelekwa Sauz

0

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Balama Mapinduzi, muda wowote kutoka leo Alhamisi anatarajia kwenda Afrika Kusini ‘Sauz’ kwa ajili ya kupata matibabu ya mguu wake wa kushoto.

 

Kiungo huyo wa zamani wa Alliance ya Mwanza, anatarajia kwenda Sauz kwa ajili ya kuangalia juu ya jeraha lake la mguu alilopata msimu uliopita mazoezini akiwa na kikosi cha Yanga katika Uwanja wa Chuo cha Sheria, Dar.

 

Daktari wa Yanga, Shecky Mngazija, amesema kiungo huyo anakwenda huko kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi zaidi wa jeraha hilo baada ya kukosekana uwanjani kwa muda mrefu.

 

“Ni kweli Balama Mapinduzi anaelekea nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kufanyiwa vipimo zaidi juu ya afya yake ili kujua maendeleo na mchakato mzima wa uponaji wa jeraha la mguu wa kushoto alilolipata baada
ya kuvunjika mazoezini.

 

“Hatuna uhakika wa muda gani atakuwepo huko kwani hilo litategemea na mpangilio wa uchunguzi atakaofanyiwa, hivyo taarifa zaidi kumuhusu tutazitoa baada ya mchezaji husika kurejea hapa nchini,” alisema Mngazija.

Stori Na SAID ALLY

Leave A Reply