The House of Favourite Newspapers

KIVAZI CHA CALISAH CHAACHA GUMZO

Calisah Abdulhamiid

Kivazi alichokivaa mwana-mitindo anayetamba Bongo, Calisah Abdulhamiid kwenye mashindano ya kumsaka Miss Tanzania 2018 yaliyofanyika hivi karibuni katika Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar kimeacha gumzo huku wengi wakisema kuwa ni cha kike.  

 

Calisah alitinga kivazi hicho cha juu chepesi mithili ya ‘night dress’ ambapo kwenye mitandao wengi walikuwa wakimsema tofauti.

“Huyu jamaa naye, ndiyo vazi gani sasa hilo la kwenda nalo sehemu kama za Miss Tanzania?” Alikomenti mtandaoni shabiki mmoja.

 

Baada ya maneno kuzagaa ambapo mjadala ulikuwa mkubwa, Showbiz Xtra lilimtafuta Calisah kuzungumzia ishu hiyo na alipopatikana alisema kuwa, sheria namba moja ya mitindo ni kuvaa chochote kile ili mradi kinamfanya mtu awe huru na mashabiki wasikariri kama kuwa mwanamitindo lazima uvae suti.

 

“Ile nguo haina vifungo na kitu pekee kinachokufanya ujue nguo kama ni ya kike au ya kiume ni vifungo na zipu vinavyowekwa upande wa kushoto au kulia. “Ilikuwa na kamba kamba za silva na ni ya kiume kabisa. Najua wanaosema hivi utawaona wakiniiga hivi karibuni,” alisema Calisah.

NEEMA ADRIAN

Comments are closed.