The House of Favourite Newspapers

KIZAAZAA! BALAA LA BUNDI ALIVYOTUA BUNGENI, SPIKA HOI – VIDEO

Katika hali isyo ya kawaida Ndege aina ya bundi ameonekana Bungeni akiwa juu kabisa ambapo Spika wa bunge, Job Ndugai, amemshuhudia Bunge huyo laivu na kusema alipomuona alichanganyikiwa kidogo na kisha akawatoa hofu Wabunge kuwa kwa Dodoma kumuona ndege huyo mchana si tatizo isipokuwa ukimuona usiku ndio unaweza kuogopa.
Baada ya tukio hilo, watumishi wa Bunge waliingia ndani ya jengo hilo kwa ajili ya ukaguzi na kumuona ndege huyo juu ya paa la ukumbi wa Bunge ambapo ndege huyo hakutoka licha ya maofisa hao kutaka kumtoa, aliruka kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
Hata hivyo, haikujulikana  muda aliotoka na mahali alikoelekea lakini Spika Job Ndugai akasema ni mambo ya kawaida kwa Dodoma.
“Waheshimiwa wabunge, asubuhi tumeanza kumwona Bundi ndani ya jengo hili, lakini kwa Dodoma Bundi wa mchana hana madhara kwa hiyo ni mambo ya kawaida kabisa,” amesema Ndugai.

KITIMTIM: Bundi Alivyoingia Bungeni, Spika Amshuhudia Laivu!

Comments are closed.