The House of Favourite Newspapers

Kizimbani kwa Tuhuma za Kusafirisha Madawa

0
KESI inayowakabili vijana wawili wakazi wa Jijini Dar es Salaam, Said Shewali na Salum Athumani ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroine, imeahirishwa hadi Desemba 29, 2021.
 
Katika hati ya mashtaka iliyosomwa katika mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu imedaiwa kuwa, Novemba 25, 2021katika uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere washtakiwa hao kwa nyakati tofauti walitenda kosa hilo.
 
Mshtakiwa wa kwanza Said Shewali alikutwa akisafirisha kilo 3.85 za dawa hizo za kulevya huku Athumani yeye alikutwa akisafirisha kilogramu 3.6.
 
Hata hivyo washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi ambazo kwa kawaida husikilizwa mahakama Kuu.
Leave A Reply