The House of Favourite Newspapers

Kizz Daniel Aunguruma na EP Mpya ya Thankz Alot

0

MKALI wa muziki nchini Nigeria, Kizz Daniel ametoa EP yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Thankz Alot’, ambayo inakwenda kuthibitisha ubora wake katika muziki.

Katika EP hiyo yenye ujazo mkubwa wa ubora, inajumuisha nyimbo nne kali, maalum kwa mashabiki wake ulimwenguni mwote, ambao wamekuwa naye kwa kipindi cha takribani muongo mmoja tangu aanze muziki.

Tangu ilipoachiwa hewani EP hiyo, imeonesha kupokelewa kwa upendo mkubwa na mwitikio chanya kwa wingi katika nchi za Afrika Mashariki na kwingineko duniani.

Akitoa shukrani zake kwa mapokezi mazuri ya kazi yake hiyo, Kizz Daniel anasema: “Ninashukuru sana kwa upendo na uungwaji mkono ambao nimepata kutoka kwa mashabiki wangu katika kipindi chote kwenye karia hii ya muziki. ‘Thankz Alot’ ni njia mojawapo ya kurudisha shukrani zangu kwa mashabiki wangu. Asanteni sana.”

EP ya ‘Thankz Alot’ ina nyimbo nne za kusisimua, kila moja ikionyesha umwamba wa Kizz Daniel na mtindo wa kipekee wa muziki.

Nyimbo hizo ni pamoja na “Sooner”, “Showa”, “Too Busy to Be Bae” na “Twe Twe” ambayo Remix yake amefanya kolabo la galacha wa muziki nchini Nigeria, Davido.

EP hiyo tayari inapatikana katika digital platforms zote.

Leave A Reply