The House of Favourite Newspapers

Klopp Awaonya Mastaa Wake Dhidi ya Manchester United Leo Jumapili

0

BOSI wa Liverpool, Jurgen Klopp, amefunguka kuwa, ni lazima wajipange dhidi ya Manchester United kwani kwenye kikosi cha wapinzani wao, si Marcus Rashford pekee ndiyo mchezaji wa daraja la juu, bali wapo wengine.

Leo Jumapili, Liverpool itavaana na Manchester United katika mchezo wa wa Premier League mzunguko wa pili ukitarajiwa kuchezwa Uwanja wa Anfield.

Katika mchezo wa awali ambao Manchester United walikuwa nyumbani Old Trafford, waliibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Klopp amesema kuwa ndani ya Man United, mchezaji wa daraja la juu na wa kumchunga sio Rashford pekee, wapo wengine ndiyo maana wanatakiwa kuwa makini.

“Rashford ana uwezo wa kufunga na anafunga mabao rahisi sana, anafanya mambo mazuri uwanjani na anajua namna ya kujilinda.

“Lakini yeye sio mchezaji pekee wa daraja la juu ndani ya Man United, hivyo tunahitaji umakini mkubwa.

“Kuna mchezaji kama Bruno (Fernandes), napenda namna anavyocheza, akiwa na mpira yupo smati, unaweza kushangaa huyu hapa tu.

“Casemiro na Fred hawa wakichezaji pamoja wanakuwa bora hasa kwa kulinda, kifiziki wako vizuri na wana uwezo wa kufanya mashambulizi ya kushitukiza kama ilivyo kwa Sancho (Jadon) ndiyo maana tunatakiwa kuwa makini na Man United.

“Lakini  pia mchezo huu utakuwa mgumu japo wapinzani wetu wanatakiwa kujua matokeo hayahusiani na masuala ya top four,  zaidi hapa tunahitaji ushindi,” alisema Klopp.

HUU HAPA UKWELI WOTE KUHUSU FEI TOTO DHIDI ya YANGA na SHERIA ya FIFA ya KUVUNJA MIKATABA….

Leave A Reply