The House of Favourite Newspapers

Kocha Baraza aipa ubingwa Yanga

0

Aliyekuwa Kocha mkuu wa timu za Biashara United na Kagera Sugar  Francis Baraza ambaye kwa sasa ni kocha mkuu wa Polisi FC ya nchini Kenya amesema kutokana na mwenendo wa ligi kuu Tanzania bara unavyoendelea klabu ya Yanga SC ndiyo itakayotwaa Ubingwa wa ligi hiyo kutokana na klabu hiyo kuonyesha ushindani mkubwa tofauti na ilivyo kwa Simba na Azam ambao wamekuwa wakisuasua kupata matokeo kwenye ligi hiyo.

Baraza ambaye kwa sasa yuko kwao Kenya akiinoa Polisi fc baada ya mkataba wake Kagera Sugar kusitishwa mwaka jana amesema “Nimekuwa nikifuatilia ligi ya Tanzania na ukweli ni kwamba hii ligi ni miongoni mwa ligi bora tano Afrika kwa sasa na ushindani wake unatokana na wachezaji wengi wa kigeni ambao wanaletwa kwakua wamekuwa wakiongeza thamani na ubora wa ligi yenyewe”

“Kuhusu Ubingwa lazima niseme ukweli kwamba klabu ya Yanga sc inayo nafasi kubwa ya kutwaa Ubingwa wa ligi kuu ya NBC kwa msimu huu  kwakua ndiyo timu pekee ambayo imekuwa na mwendelezo wa kupata matokeo tofauti na Simba na Azam ambao wanashindwa kupata matokeo mfululizo jambo linaloifaidisha Yanga kuendelea kuweka uwiano mkubwa wa pointi”

“Ukiwatizama Yanga SC  wana vijana wengi ambao wanaisaidia timu mfano kama Clement Mziza ambaye anafunga kila akipewa nafasi  hivyo kwa msimu huu haina ubishi kwamba Yanga itachukua Ubingwa mbele ya Simba na ili Yanga iache kuwa bingwa lazima Simba wajipange kufanya zaidi ya kile ambacho Yanga wanakifanya cha kuwa na timu bora”

Leave A Reply