The House of Favourite Newspapers

Kocha Brazil Atimuliwa Kazi Baada ya Kumpiga Kichwa Mwamuzi wa Kike

0
         Meneja wa Desportivo Rafael Soriano akimpiga kichwa mwamuzi wa kike Marcielly Netto

KOCHA wa Klabu ya Desportivo Ferroviaria  inayoshiriki daraja la tano nchini Brazil Rafael Soriano ametimuliwa kazi baada ya kumpiga kicwa mwamuzi wa pembeni na kusababisha kumpasua pua.

 

Tukio hilo limetokea katika pambano la robo fainali kati ya Desportivo Ferroviaria dhidi ya Nove Venecia ambapo Nova walishinda kwa jumla ya mabao 3-1.

                        Mwamuzi msaidizi Marcielly Netto alipoingilia kumzuia kocha wa Desportivo

Kocha wa Desportivo Rafael Soriano aliingia uwanjani baada ya kipindi cha kwanza kumalizika akienda kupinga maamuzi ya mwamuzi wa kati wa mchezo lakini mwamuzi msaidizi mwanadada Marcielly Netto akaingilia kati ili kumzuia ndipo hapo alipoambulia ndoo ya maana na kupasuka pua.

 

Mara baada ya tukio hilo Klabu ya Desportivo Ferroviaria ilitoa taarifa ya kumtimua kazi kutokana na kitendo hicho.

 

 

 

Leave A Reply