The House of Favourite Newspapers

Kocha Kaze Kurejea Bongo Tena

0

INAELEZWAaliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga, Mrundi, Cedric Kaze ameondoka nchini kurejea kwao Burundi kwa ajili ya mapumziko mafupi kabla ya kurejea tena nchini kwa lengo la kufanya mipango ya kueleka nchini Canada.

 

Kaze ameondoka nchini baada ya kutimuliwa Yanga akiwa na wasaidizi wake, Vladimir Niyonkuru na Nizar Khafan kutokana na mwenendo wa matokeo sare za mfululizo ndani ya timu hiyo ikiwemo kupoteza mchezo mmoja dhidi ya Coastal Union.

 

Hivi karibuni staa mwingine wa Yanga, Said Ntibazonkiza ‘Saido’ aliyesajiliwa Kaze kikosini humo alikuwa wa kwanza kurejea Burundi kwa ajili ya majukumu ya mechi za kimataifa.

 

Kwa mujibu wa taarifa ambazo Championi limezipata kutoka kwa mtu wa karibu wa kocha huyo alisema kuwa, Kaze amerejea Burundi kwa ajili ya mapumziko mafupi lakini amepanga kurejea tena nchini ili kuweza kufanya mipango yake mingine.

 

“Mwalimu Kaze ameshaondoka lakini amekwenda Burundi kwa ajili ya kuangalia ndugu na kuweka sawa mambo yake mengine kwa sababu hakuwepo kule kwa muda mrefu.

 

“Lakini atarudi tena hapa Dar es Salaam kwa sababu bado hajamaliza kuweka sawa baadhi ya mambo yake, ila safari yake ya kurejea tena Canada itaanzia hapa kwa kuwa kila kitu chake kipo hapa hivyo hana muda mrefu atakuwa amerejea licha ya kutoweka wazi itakuwa ni siku gani,” alisema mtoa taarifa.

STORI NA IBRAHIM MUSSA NA HAWA ABUBAKAR

Leave A Reply