The House of Favourite Newspapers

Kocha Mpya Mcongo Aliamsha Dude Yanga

Kocha Mkuu mpya wa Yanga, Mcongo Za­hera Mwinyi.

AKIANZA kukinoa kwa mara ya kwanza, Kocha Mkuu mpya wa Yanga, Mcongo Za­hera Mwinyi amekiangalia kikosi hicho mazoezini kwa saa mbili na kutamka kuwa amevutiwa na viwango vya wachezaji aliowakuta huku akisema shughuli imeisha.

 

Kocha huyo alitua nchini alfajiri ya Jumapili iliyopita akitokea Kongo kwa ajili ya kuifundisha timu hiyo akirithi mikoba ya Mzambia, George Lwandamina aliyesitisha mkataba wake wa kuendelea kukinoa kikosi hicho kabla ya kujiunga na Zesco ya Zambia.

Mkongoman huyo mwenye uraia wa Ufaransa mara baa­da ya kutua nchini aliomba kwenda kuiona timu hiyo kambini Morogoro ilipoku­wepo timu hiyo ikijiandaa na mchezo wa watani wa jadi, Simba utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

 

Akizungumza na Cham­pioni Ijumaa, Zahera alisema ameshangazwa na viwango hivyo vya wachezaji alivyovikuta huku akivutiwa na fitinesi, pumzi ambavyo ndiyo vitu muhimu kwenye timu katika kupata ushindi.

Amesema baada ya kuona viwango vya wachezaji katika kuelekea mechi dhidi ya Sim­ba amepanga kuwaongezea vitu viwili ili kuhakikisha Yan­ga inapata matokeo mazuri katika mchezo huo wa watani wa jadi ambavyo ni mbinu za kulinda na kushambulia na mfumo wake.

 

“Kama unakumbuka mara ya mwisho tulivyoon­gea hotelini kabla ya kuja kambini Morogoro, niliomba niende nikaitazame kwanza timu baada ya hapo men­gine yafuate ya mimi kusaini mkataba wa kuifundisha.

 

“Hicho ndicho nilichoki­fanya, nashukuru nimefika kambini salama na haraka nikaanza kuifundisha timu kwa saa mbili kwa ajili ya kuangalia kikosi, lakini imekuwa ‘sapraizi’ kwangu kukuta wachezaji wengi vi­jana wenye uwezo mkubwa.

 

“Kwa siku hizi tatu nitaka­zokaa na timu kambini kwa ajili ya kujiandaa na mechi zitatosha kwangu ku­waongezea baadhi ya vitu vi­chache nilivyoviona ambavyo wachezaji wangu wanahitaji kuongezewa, sitaki nikivu­ruge kikosi,” alisema Zahera.

Stori: Wilbert Moland ina Musa Mateja

Comments are closed.