The House of Favourite Newspapers

KOCHA MPYA YANGA AANZA KIVINGINE

MUDA mfupi baada ya kukabidhiwa kijiti cha kuiongoza Yanga baada ya kuondoka kwa George Lwandamina, kocha mkuu mpya wa timu hiyo, Noel Mwandila, amesema mechi yao na wapinzani wao Simba haipo kwenye hesabu zake kwa sababu anataka kwanza kuiona timu hiyo inapenya kwenye hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Mwandila amekabidhiwa mikoba ya ukocha mkuu wa timu hiyo ikiwa ni baada ya jina lake kupitishwa na kamati ya utendaji ya timu hiyo ambayo ilikutana wiki iliyopita kwa ajili ya kujadili nafasi ya Lwandamina ambaye ametimka kwenye kikosi hicho na inatajwa kuwa ataifundisha Zesco United baada ya kusaini nayo mkataba.

 

Akizungumzia juu ya mechi hiyo na Simba, Mwandila raia wa Zambia alisema: “Kwa nini unaniuliza juu ya mechi ambayo kwa sasa haipo katika hesabu zangu? Hiyo mechi iko mbali sana (Aprili 29, mwaka huu) tofauti na kuniuliza vitu ambavyo vipo karibu mbele yetu.

“Kwangu mimi siifikirii mechi hiyo bali ninachokita­zama ni kuhakikisha kwamba tunapata ush­indi mbele ya mchezo wetu na Wolatya Dicha ambayo tutacheza Juma­tano tukiwa ugenini, lab­da nikishamaliza hapo na tukifanikiwa kupata ushindi na kusonga mbele ndipo uje uniulize juu ya mechi hiyo.

 

“Kushinda na kusonga mbele katika Kombe la Shirikisho ni muhimu zaidi kuliko kuingiza mambo mengine hapa kati kwa sasa, mawazo na akili zetu ni kuona Yanga inasonga mbele kwenye kombe hili kisha ndipo tudili na mashindano men­gine.”

Mwandila ambaye ni kocha mbobezi wa mazoezi ya viungo, ataiongoza Yanga Ju­matano kuhakikisha haifungwi zaidi ya bao 1-0 ili kusonga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, baada ya wiki moja iliyopita kushinda 2-0 dhidi ya Dicha kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.

Said Ally na Musa Mateja.

Comments are closed.