The House of Favourite Newspapers

Kocha Mrundi: Kwa Onana, Simba Imelamba Dume

0
Willy Onana akifanya yake.

KOCHA wa zamani wa Simba na Dodoma Jiji, Masoud Djuma, amemwaga sifa za kutosha kwa winga mpya wa Simba, Willy Onana akisema ni mtu hatari uwanjani.

Onana raia wa Cameroon amejiunga na Simba akitokea Rayon Sports ya Rwanda, ambapo alikuwa na mafanikio makubwa baada ya kumaliza ligi akiwa kinara kwa kutupia mabao 16.

Masoud Djuma

Akizungumza na Championi Ijumaa, Masoud Djuma alisema kuwa Onana ni mchezaji hatari sana na anastaili nyingi za uchezaji bora zaidi ya Saido Ntibazonkiza na Pape Sakho.

“Onana ni msikivu sana ila pia ni hatari sana uwanjani hasa kwa kufunga, ila pia ni msikivu sana linapokuja suala la maelekezo kwa kocha hivyo ninaimani atafanya vizuri sana kwa Simba,” alisema Masoud.

Stori na Musa Mateja, Championi

WAZIRI MKUU MAJALIWA – “BANDARI ya MTWARA INAKWENDA KUWA KUBWA KULIKO ZOTE”, AANIKA MIPANGO

Leave A Reply