The House of Favourite Newspapers

Kocha Simba Akomalia Tizi la Mabao ya Mbali

0

KOCHA wa Simba, Didier Gomes, amesema kuwa moja kati ya programu ambayo anaitilia mkazo kwa sasa akiwa Morocco ni wachezaji wake kufunga mabao ya mbali.


Gomes alisema kuna kazi
nyingi za kufanya akiwa Morocco, lakini kubwa zaidi ni timu kuweza kufunga kwa kila namna ikiwemo nje ya boksi la wapinzani kwani kwa kufanya hivyo watakuwa na njia nyingi za kupata ushindi wakati wa mechi.

Simba kwa sasa ipo Morocco ilipoweka kambi ya kujiandaa na msimu wa 2021/22 ambapo ipo huko tangu Jumatano wiki hii.

Akizungumzia maendeleo ya kambi hiyo, Gomes alisema kila kitu kinakwenda vizuri kutokana na mazingira yalivyo na kwa sasa wanaangalia namna nzuri ya timu kutimiza kila program waliyoiweka.

“Kambi ipo vizuri kutokana na nchi ambayo tupo hali ya hewa yake kuwa nzuri kwetu, kambi hii ina faida nyingi kwa sasa, tunaagalia zaidi wachezaji kufunga nje ya boksi, tunajaribu kuangalia namna gani vijana watafanyia kazi eneo hilo kwa sasa,” alisema Gomes

Leave A Reply