The House of Favourite Newspapers

Kocha Simba: Kwa Balinya, Yanga imelamba dume

KOCHA wa zamani wa Simba, Mganda Jackson Mayanja amesema Yanga imelamba dume kwa kumsaini mshambuliaji, Juma Balinya ambaye naye ni Mganda. Hivi karibuni Yanga ilimsajili Balinya akitokea Polisi ya Uganda aliyokuwa akitumikia msimu uliopita na kuweza kuifungia mabao 19 yaliyomwezesha kuwa mfungaji bora wa ligi hiyo.

 

Mayanja ambaye juzi alitambulishwa kuwa kocha wa KMC, aliliambia Championi Jumamosi kuwa, Balinya ni mmoja kati ya washambuliaji chipukizi wa Uganda ambao wanakuja vizuri hivyo uwepo wake ndani ya Yanga utaifanya timu hiyo iwe moja kati ya timu tishio.

 

“Ninamjua vizuri sana Balinya, ni mchezaji mzuri ambaye anajua sana kufunga anapokuwa uwanjani. Uganda alikuwa akicheza katika timu ya chini sana lakini ameibuka mfungaji bora tena mbele ya washambuliaji mahiri wa timu kubwa kama SC Villa, KCCA na nyingine nyingi.

 

“Niwapongeze tu Yanga kwa usajili huo, naamini hawataujutia kwani Balinya ni mchezaji mzuri na anayejituma vilivyo uwanjani,” alisema Mayanja kuongeza kuwa. “Jambo kubwa ambalo ninaweza kuwashauri Yanga, wampatie tu ushirikiano kama ambavyo wamekuwa wakifanya kwa washambuliaji wengine waliopita.”

KATA MBUGA: DADA ASIMULIA MKASA WA KUZAMIA INDIA, KUFANYA KAZI YA KUJIUZA

Comments are closed.