The House of Favourite Newspapers

KOCHA YANGA APATA KIBURI LIGI KUU BARA – VIDEO

Mshambuliaji wa Yanga, Heritier Makambo akipongezana na Mrisho Ngassa (kulia).

MABAO 11 waliotupia mastraika wa Yanga kwenye mechi sita yamempa kiburi, Kocha Mkongomani Mwinyi Zahera.

“Ukiangalia kwenye mechi sita timu imefunga mabao 11 hakuna timu ligi ambayo imefanya hivyo kwenye mechi zao sita ambazo wamecheza.

 

“Hivyo washambuliaji wangu niseme ni bora kuliko wengine sababu hakuna aliyewafikia ila hawapaswi kuridhika bado wana safari ndefu na wanahitaji kupambana na kufanya kweli kwa kufunga mabao kwa kila mchezo ambao watacheza,” alisema Zahera.

STORI NA MARTHA MBOMA

Comments are closed.