The House of Favourite Newspapers

Kocha Zahera Amwaga Machozi Yanga

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, raia wa DR Congo, amefunguka kuwa wachezaji wake ni wavumilivu na amekuwa akiwasikiliza kila mara mpaka machozi yanamtoka kutokana na matatizo waliyonayo licha ya kuwa mashabiki wamekuwa wakiwasema bila kujua wanapitia hali gani.

 

Yanga imekuwa ikipitia nyakati ngumu hasa kiuchumi tangu mwishoni mwa msimu uliopita hali ambayo inadaiwa ilichangia wao kutofanya vizuri ingawa msimu huu mpaka sasa imekuwa ikipambana kufanya vizuri chini ya Mkongo huyo.

Mkongo anayejulikana kwa ‘kutoumauma’ maneno, amese­ma anatamani kuona mashabiki wa timu hiyo wakitembelea mazoezi ya timu hiyo na kupata nafasi ya kuzungumza na wache­zaji kujua nini kinawasumbua.

 

“Katika wachezaji ambao nime­wahi kufanya nao kazi wachezaji wangu hawa wa Yanga ni wavu­milivu sana, kuna wakati huwa nawasikiliza mpaka machozi yananitoka kutokana na matatizo ambayo yanawakabili.

“Lakini bado mashabiki hawa­hawa wamekuwa wakiwanyooshea vidole na kuwasema vibaya saba­bu hawajui wachezaji wanapitia vitu gani na ninaomba mashabiki wetu wa Yanga waje hata katika mazoezi ya timu wapate kuon­gea na wachezaji wao wajue nini kinawakabili.

 

“Sababu hawajui huenda wakau­mia kwa kuwa walikuwa wana­niambia kocha sisi tunaumizwa na matokeo ya wachezaji wetu lakini hawajui wachezaji wanapitia matatizo gani, wajaribu kuwasiki­liza wachezaji labda na wao roho zitawauma.

“Wachezaji wanaendelea na magumu yao huku mashabiki nao wanasema waendelea kupambana na Tanzania mashabiki wa mpira ni wengi ila wanataka kuongozwa kwa miujiza ya Mungu jambo am­balo ni gumu,” alisema Zahera.

 

Zahera tangu aanze kukinoa kikosi hicho, msimu huu katika mechi 10 hajapoteza mchezo hata mmoja na amefanikiwa ku­toa sare mechi mbili na timu ina pointi 26 sawa na Simba.

Hivi karibuni kocha huyo alinukuliwa kuwa yeye ataende­lea kuifundisha Yanga bila kujali analipwa kiasi gani sababu mai­sha siyo fedha peke yake.

Martha Mboma, Dar es Salaam

Zuku na Mobisol Waja na TV zinazotumia Umeme wa jua

Comments are closed.