The House of Favourite Newspapers

Kodi Zamrudisha Ninja Yanga

0

NAELEZWAbeki wa kimataifa wa Tanzania, Abdallah Shaibi ‘Ninja’ amekubali kurejea nchini kujiunga na Yanga kufuatia kushindwa kuvumilia makato ya kodi katika mshahara wake huko Jamhuri ya Czech.

 

Beki ambaye alijiunga na Klabu ya MFK Vyskov inayoshiriki Ligi Daraja la Tatu nchini humo kabla ya kumtoa kwa mkopo katika LA Galaxy aliyokuwa akitumia nyota wa zamani wa Manchester United, Zlatan Ibrahimovich lakini hakuweza kudumu akarejea kwenye timu yake kabla ya juzi kuibukia mazoezi ya Yanga.

 

Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika ni kuwa, beki huyo ameamua kurejea nchini kutokana na kushindwa kuvumilia makato ya kodi aliyokuwa akikatwa kwenye mshahara wake nchini humo.

 

“Yanga wamekuwa naye kwenye mazungumzo ya kumrudisha na yote wameanza kujipanga kwa ajili ya msimu ujao wa ligi lakini kuna mambo bado hawajafikia muafaka kutokana na Ninja mwenyewe anavyotaka mkataba wake uwe.

 

“Kikubwa kilichomrudisha ni kodi, mwenyewe anasema lilikuwa ni jina kwamba anacheza nje ya Tanzania lakini katika upande wa maslahi kwake imekuwa ni changamoto kutokana na kodi kubwa tofauti na anachoingiza ndiyo maana ameona arejee nyumbani,” kilisema chanzo.

Stori: Ibrahim Mussa, Dar es salaam

Leave A Reply