The House of Favourite Newspapers

Kofi Annan Kuzikwa Leo Jijini Accra

Kofi Annan

MWILI  wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan, unatarajiwa kuzikwa leo katika mji mkuu wa Ghana, Accra. Kwa muda wa siku mbili zilizopita mwili wake ulikuwa ukiagwa mjini humo na watu mbalimbali, wakiwemo watu maarufu.

Viongozi kadhaa wa nchi wanatarajiwa kuhudhuria mazishi hayo katika makaburi ya jeshi ya Kambi ya Burma mjini Accra.   Kofi Annan alishika nafasi hiyo akiwa Katibu Mkuu wa saba wa Umoja wa Mataifa kati ya 1997 na 2006.

Leo ni kilele cha wiki kadhaa za maandalizi ya maziko yake akiwa mmoja wa wanadiplomasia walioheshimika duniani.

Mwandishi wa BBC aliyeko mjini Accra amesema ngoma za maombolezo zilisikika mfululizo kwa muda wa siku mbili katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Accra, sehemu ambayo mwili wake ulikuwa ukiagwa na watu mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.Wanajeshi wakiwa wameubeba mwili wa Kofi Annan ulipowasili Ghana Jumatatu wiki hii

Miongoni mwa waombolezaji waliwasili mjini humo ni aliyewahi kuwa mke wa rais wa kwanza wa Afrika kusini Nelson Mandela, Bibi Graca Machel.     Marais na viongozi kutoka maeneo mbalimbali ya Afrika ikiwemo Ivory Coast, Ethiopia na Zimbabwe watahudhuria maziko hayo.   Pia wamo marais wa zamani wa Ujerumani, Finland na Uswizi.

Shughuli hiyo ya kumuaga marehemu itafuatiwa na maziko yatakayofanywa kwa ndugu wa karibu na kwa heshima zote za kijeshi.Machifu, wanasiasa na jamaa wanaonekana wakisubiri kutoa heshima zao za mwisho kwa Kofi Anna katika lango la kuingia ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Accra Jumatano

Wachezaji ngoma wa jamii ya Ashanti wakati wa ibada iliyofanyika Jumatano

Comments are closed.