Vyuo Vikuu 10 Bora Zaidi Barani Afrika
1 University of Cape Town – Cape Town, South Africa
The University of Cape Town (UCT), kiko katika miteremko ya mlima uitwao Devil’s Peak jijini Cape Town, kikiwa ndicho chuo kikuu kikongwe zaidi nchini Afrika Kusini. Kilianzishwa mwaka 1829 na kina wanafunzi zaidi ya 25,000 walimu wapatao 1,000.
2 American University in Cairo – Cairo, Egypt
Kilianzishwa mwaka 1919 huchukua wanafunzi wapatao 16,000 kila mwaka.
Miongoni mwa wahitimu wake maarufu ni waziri wa zamani wa ulinzi wa Japan, Yuriko Koike, mwanadiplomasia na mwandishi wa habari wa Romania, Dan Stoenescu, na mtayarisha filamu wa kwanza wa kike wa Saudi Arabia, Haifa Al-Mansour.
3 Al Akhawayn University – Ifrane, Morocco
Kilianzishwa mwaka 1995 kikiwa kimejengwa katika eneo la Milima ya Atlas.
4 University of Nairobi – Nairobi, Kenya
Kilianzishwa 1956 ambapo pamoja na kuchukua wanafunzi wapatao 70,000, kina walimu wapatao 1,600 na huchukua wastani wa wanafunzi 120 kutoka nchi za nje kila mwaka.
5 Makerere University – Kampala, Uganda
Kilianzishwa 1922 na huchukua wanafunzi zaidi ya 40,000 kila mwaka. Ni chuo kikuu kikongwe zaidi nchini Uganda.
6 University of Ghana at Legon – Accra, Ghana
Kikiwa kilianzishwa kama tawi la University of London, baadaye kikajitegemea mwaka. Huchukua wanafunzi zaidi ya 38,000 kila mwaka.
7 University of Ibadan – Ibadan, Nigeria
Kilianzishwa 1948, kiko pembeni mwa jiji la Ibadan. Kinajulikana pia kama Unibadan au UI.
8 University of Botswana – Gaborone, Botswana
Kilianzishwa 1982, kikiwa na makazi matatu ya wanafunzi (campuses) katika jiji la Gaborone, Francistown na Maun. Huchukua wanafunzi karibu 19,000 kwa mwaka.
9 University of Dar es Salaam – Dar es Salaam, Tanzania
Kilianzishwa 1961 kama tawi la University of London baadaye kikawa mshiriki wa University of East Africa (UEA) mwaka 1963 baada ya Tanganyika kupata uhuru kutoka kwa Uingereza. Mwaka 1970 UEA ikagawanyika na kuanzisha vyuo vikuu vitatu vyenye kujitegemea vya Makerere University cha Uganda, University of Nairobi cha Kenya, na University of Dar es Salaam.
10 Addis Ababa University – Addis Ababa, Ethiopia
Addis Ababa University (AAU) kilianzishwa 1950 kama University College of Addis Ababa (UCAA) kikiwa na wanafunzi 33 ambapo sasa kina wanafunzi 48,673.
Tangu kuanza kwake, wanafunzi zaidi ya 222,000 wamehitimu hapo.
Comments are closed.