The House of Favourite Newspapers

Kombe La FA Ndani Ya Azam TV

KATIKA kuhak­ikisha Azam TV inakidhi mahita­ji na matakwa ya wa­teja wao, Kampuni ya Azam Media itaanza kurusha matangazo ya mechi za Kombe la FA la England.

 

Michuano hiyo inatarajiwa kuanza katika hatua ya tatu Januari 4, mwakani ambapo baadhi ya mechi zitakazoonyeshwa ni Man United v Reading, Wolves v Liverpool , Man City v Rotherham, Chelsea v Nottingham Forest na mshindi kati ya Solihull Moors na Blackpool v Arsenal.

 

Azam itaungana na wapenda soka duniani kote kukuletea michuano hiyo mikongwe iliyoanzishwa mwaka 1871.

Kombe la FA maarufu kama Emirates, huzikutanisha timu za madaraja mbalimbali England.

 

“Hii ni hatua nyingine muhimu ambayo Azam TV tumechukua kuhakikisha wateja wetu wanafurahia burudani ya soka sebuleni kwao na popote walipo. “Hata kupitia simu zao za kiganjani ‘Smartphone’ kupitia programu tumishi ya Azam TV App inayopatikana bure bila malipo yoyote.

Hakika hii ni zawadi tosha ya mwisho wa mwaka kwenu wateja wetu wa Azam TV,” alisema Mkurugenzi wa Azam TV, Tido Mhando.

Comments are closed.