The House of Favourite Newspapers

Kopa Atoa Mbinu za Mwanamke Kujikwamua

0
Mwanamuziki mashuhuri wa miondoko ya Taarab, Afrika Mashariki, Khadija Kopa.

 

MAMBO vipi mpenzi msomaji wa safu hii Ulipo Mwanamke Tupo (UMT).

Wiki iliyopita tulikuwa naye msanii mkongwe wa filamu Bongo, Fatuma Makongoro ‘Bi Mwenda’ lakini leo tunaye mwanamuziki mashuhuri wa miondoko ya Taarab, Afrika Mashariki, Khadija Kopa.

Ameeleza siri ya mafanikio yake hadi kufikia hatua ya kuwa na jina kubwa:

UMT: Bi.Khadija wengi wangependa kufahamu ni mikiki gani ulikutana nayo mpaka leo hii upo na unaendelea kuwa juu?

KOPA: Changamoto na hekaheka ni nyingi lakini yote nafikiri nilishinda kwa sababu nia ni moja tu, kufikia malengo.

Mwanamke unatakiwa kujiamini, jipe nguvu. Utafanikiwa.

UMT: Kama mwanamke ulikuwa ukipewa

sapoti na nani mpaka kufikia hapa?

KOPA: Hakuna msaada mkubwa nilioupata kwa mtu zaidi ya kujiamini. Ni muhimu sana kujiamini, najikubali kuliko kitu chochote na ndio maana nimeweza kusonga mbele bila woga.

Akifanya yake.

UMT: Watu wengi wakikuona ni mwanamke huwa wanatumia nafasi hiyo kumuonea kijinsia, hiyo kwako ikoje?

Kopa: Kiukweli nilikuwa ngangari ni mwanamke wa shoka, najua kukomaa na ndiyo maana hata waliokuwa wanataka kunionea waliingia mitini.

UMT: Zamani najua marehemu mumeo (Jaffari Ally) alikuwa akikupa nguvu zaidi na kampani kubwa, umewezaje kuendelea mwenyewe bila kuyumba?

KOPA: Ni kujipa moyo tu kwa maana kuna kipindi nilipambana mwenyewe hata kabla ya kuolewa na mume wangu yaani kifupi mimi ni jembe.

Niwasihi na wengine waliopoteza waume zao, wasikubali hata mara moja kukatishwa tamaa, wasimame na waamini Mungu yupo atawatetea.

UMT: Ulipoteza mume wako lakini mashabiki wako wanatamani kujua unatarajia kuolewa tena au ndiyo basi tena?

Kopa: Kwa nini niseme sitaolewa tena na mimi ni mwanamke, kikubwa ni kumuomba Mungu akuletee mume bora kama aliyepita.

UMT: Ni ushauri gani unawapa wanawake ambao ni wapambanaji katika maisha?

KOPA: Niwashauri wanawake wenzangu tujifunze kujisimamia na kujiamini kwa kila jambo. Fanya kile unachoona unaweza kukifanya, jiamini na utafanikiwa tu.

UMT: Ni mafanikio gani umeyapata kutokana na kazi yako hiyo:

KOPA: Mafanikio ni mengi sana jamani siwezi kuyataja moja kwa moja lakini itoshe tu kusema si haba, namshukuru Mungu kwa hilo.

UMT: Ni staa gani mwanamke ambaye anakuvutia Bongo?

KOPA: Ni yule ambaye anajituma na kujijeshimu kama mwanamke maana lazima mwanamke uwe na staha.

UMT: Zaidi ya muziki kuna kitu kingine unafanya cha kukuongeze kipato?

KOPA: Ndiyo, nina biashara zangu ndogondogo, nawashauri pia wanawake wenzangu waanzishe vibiashara vidogovidogo, vinasaidia kwenda kwenye biashara kubwa. Unaweza kuuza vitumbua, genge au hata Ice Cream.

Taratibu utakuza mtaji na kuweza kufanya biashara hata ya nguo na baadaye hata duka au saluni.

UMT: Nakushukuru sana Kopa.

KOPA: Karibu tena!

Fainali ya Shinda Nyumba… George Majaba wa Dodoma Ajinyakulia Nyumba

Leave A Reply