The House of Favourite Newspapers

KRISMASI ILIVYONOGA DAR LIVE; HAKUNA ALIYELALA (Picha + Video)

Christian Bella akiwanogesha mashabiki wake.
Wanenguaji wa Malaika Band wakiwajibika.
Christian Bella akiwaimbisha kinamama wimbo wa ‘Nani kama mama’.
Mdada kibonge aliamua kwenda kujiachia n Bella ‘kwa sana’.
Vairas Mdudu Mmoja akiimba na kuwapa ‘Hi’ mashabiki wake.
Kiongozi wa Kundi la First Class Modern Taarab, Mfalme Amigo(katikati),   na waimbaji wake.
Mpapasa kinanda mahiri, Ally Jay, akifanya yake katika kuwakuna mashabiki.
Mashabiki ‘waliokunwa’ na swaga za Yuda Msaliti (kushoto) waliamua kuvamia jukwaa na kwenda kumsapoti.
Mosi Suleiman wa First Class akiwapa mashabiki ‘kitu roho inapenda’.

WAPENZI wa burudani usiku wa kuamkia leo walishuhudia shoo ya nguvu kutoka kwa makundi mbalimbali ya burudani ambapo kundi la First Class Modern Taarab chini ya Mfalme Amigo ndilo lililofungua pazia la burudani kisha kumpisha kwa muda Mfalme wa Masauti, Christian Bella ‘Obama’,  aliyekuwa na Malaika Band.

Wapenzi wa singeli nao ilikuwa siku yao ya kupasha misuli baada ya Vairas Mdudu kuvamia jukwaa na kisha kumuachia jukwaa Yuda Msaliti ambaye baada ya kuwapeleka ‘mpesempese’ mashabiki wa burudani na aliwapisha tena First Class ambao walifunga shoo muda wa kufungulia kuku.

Mchanganyiko huo wa burudani ulionekana kumfanya kila mtu akate kiu yake ya burudani.

HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS / GPL 

Prince Amigo Akikiwasha Muda Huu Dar Live

BALAA LA CHRISTIAN BELLA STEJINI DAR LIVE

Comments are closed.