The House of Favourite Newspapers

Kuelekea Tamasha La Tuzo Za Filamu Kesho Jumamosi, Mastaa Na Wadau Wafanya Kongamano

0
Mastaa wa filamu kutoka kushoto, Single Mtambalike ‘Rich’, JB na Batuli wakifuatilia yanayoendelea kwenye kongamano hilo. 

Dar es Salaam 15 Desemba 2023: Bodi ya filamu nchini katika kuelekea kwenye Tamasha la Tuzo za filamu nchini kesho Jumamosi, imefanya kongamano na wadau wa filamu na kujadili maslahi ya kazi hiyo.

Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu, Dk Kiagho Kilonzo akizungumza na wanahabari (hawapo pichani).

Katika kongamano hilo wasanii na wazalishaji wa filamu walitoa mapendekezo kwa bodi hiyo kama serikali ikayapokea na kuwaahidi kuyafikisha serikali kuu kwa ajili ya kuyafanyia kazi.

Wadau kwenye kongamano hilo.

Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika Ukumbi wa Super Dome uliopo Masaki jijini Dar ambapo mastaa wa filamu karibu wote wanatarajiwa kuhudhuria.

Mchekeshaji Joti (katikati) pamoja na mabo yake yote lakini kwenye ishu za msingi huwa makini sana kusikiliza kama ilivyokuwa leo kwenye kongamano hilo. Kushoto ni Rado na kulia ni Wellu Sengo.

Kwa upande wa Serikali Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Dk. Kiagho Kilonzo na maofisa wa bodi hiyo ndiyo walioiwakilisha serikali kujibu hoja za wadau wa filamu waliofurika kwenye kongamano hilo.  HABARI/PICHA NA RICHARD BUKOS WA GLOBAL TV

Leave A Reply