The House of Favourite Newspapers

Kumbe bibi alimbadilisha Will Smith asitukane kwenye nyimbo zake

0
MIAMI, FL - FEBRUARY 04:  Will Smith is on the set of Despierta American to promote his film "Focus". at Univision Studios on February 4, 2015 in Miami, Florida.  (Photo by Gustavo Caballero/Getty Images)
                                               Will Smith akiwa katika pozi

Imebainika kuwa bibi wa staa wa muziki na filamu anayekimbiza Hollywood, Will Smith alimfanya asiingize matusi ya aina yoyote katika nyimbo zake. Unajua ilikuwaje?

rs_634x846-150212125044-Will-Smith-esquire

Katika interview aliyofanyiwa mwishoni mwa mwaka 2015 rapa Will Smith alisema;

“Nilianza kupenda na kutaka kurap nikiwa na miaka 12,nilianda kuandika mashairi mwaka huo kwenye kitabu changu kidogo ”

Akaanika siri ya bibi yake sasa;

“Bibi yangu alikuta kitabu changu cha mashairi na kusoma baadhi y nyimbo zangu,hakusema lolote ila alichukua kitabu hicho na kuandika nyuma kabisa kwenye kurasa ya mwisho, Dear Willard ‘Truly intelligent people do not have to use words like this to express themselves. Please show the world that you’re as smart as you think you are’ akimaanisha watu wenye uwezo mkubwa wa kufikiria hawatumii maneno kama haya kuelezea mitazamo yao, tafadhali onyesha dunia unaakili kama unavyofikiria. Tangu siku hio sikuwahi kupanga kutukana kwenye muziki wangu,” akaweka nukta.

(Imeandaliwa na Andrew Carlos/GPL)

Leave A Reply