The House of Favourite Newspapers

Kumbukumbu ya Kifo cha Baba Mzazi wa Eric Shigongo Yafanyika Dar

0

Agosti 25, 2017 (jana), ilitimia miaka mitano tangu kufariki kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Kampuni ya Global Publishers & General Enterprises Ltd, James Bukumbi, ambapo ilifanyika  ibada fupi ya kumuombea nyumbani kwa mjane wake, Asteria Kapera, Mikocheni jijini Dar.

Katika ibada hiyo, Mkurugenzi  wa kampuni hiyo, Marsha Bukumbi alitoa neno la nasaha kwa ndugu, jamaa na marafiki kwamba yatupasa kuwapenda wazazi wetu na kumpendeza Mungu.

Ibada hiyo ya kumbukumbu iliongozwa na Padri Gideon Rwezahura ambaye ni Paroko wa Parokia ya Mikocheni akisaidiana na Padri Yudathadei Tenga wote kutoka Parokia ya Mikocheni, Dar.

Katika mafundisho yake, Padri Rwezahura amewaasa waumini kumuweka Mungu mbele katika maisha yao ya kila siku na kutenda matendo mema huku akitumia muda mwingi kuwafariji wanafamilia, ndugu na jamaa waliohudhuria kuwa marehemu James Bukumbi yuko mahali salama na wazidi kumuombea.

Viongozi wa dini walioongoza misa ya kumuombea marehemu Bukumbi.

                                   Ndugu, jamaa na marafiki waliohudhuria misa hiyo.

Padri Gideon Rwezahura akimuombea mjane wa marehemu, Asteria Kapera.

 

 

 

Marsha Bukumbi (wa kwanza kulia), akifuatilia jambo kwenye misa hiyo.

Padri Gideon Rwezahura (kulia) wa Parokia ya Mikocheni akiwa na Padri Yudathadei Tenga.

Leave A Reply