The House of Favourite Newspapers

KUTOKA IRINGA: Miili ya Maria na Consolata Yaagwa – Video

  
MIILI ya mapacha Maria na Consolata Mwakikuti (20) waliofariki dunia Jumamosi iliyopita katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa, imeagwa katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ruaha (RUCU) kabla ya kuzikwa katika makaburi ya viongozi wa dini yaliyopo Tosamaganga mkoani humo leo Jumatano, Juni 6, 2018.

 

Maria na Consolata ambao enzi za uhai wao walikataa kutenganishwa, watazikwa kwenye jeneza moja litakalokuwa na misalaba miwili.

 

Familia za baba na mama wa mapacha hao kutoka Tukuyu, Mbeya na Bukoba, Kagera, waliokuwa walezi wa mapacha hao, masista wa Consolata wa Iringa, na waombolezaji wengine,  wameungana katika kuwasindikiza mapacha hao katika safari yao ya mwisho duniani.

Shughuli za kuaga miili hiyo imeanza saa mbili asubuhi katika chuo cha Rucu ambapo baadaye msafara wa maziko utapita barabara kuu kuelekea Tosamaganga ili wananchi ambao hawatafika Rucho waweze kutoa heshima zao za mwisho.

 

VIDEO: SHUHUDIA TUKIO HILO LA KUAGA HAPA

Comments are closed.