The House of Favourite Newspapers

Harmonize Kufanya Show Babkubwa Dar Live Idd Pili

Msanii wa muziki kutoka WCB, Harmonize (katikati) akiwa na Meneja wa burudani, Rajabu Mteta ‘KP Mjomba’ (kulia).

 

MSANII kutoka kwenye kundi la Wasafi Class Baby (WCB), Rajabu Abdul Kahali ‘Harmonize’ kwa kushirikiana na Global Group, anatarajia kutoa shoo babkubwa siku ya sikukuu ya Idd Pili kwenye Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live, Mbagala.

 

Akizungumza na Cham­pioni Jumatano, Harmonize alisema kuwa siku ya Idd Pili atafanya shoo yake ya kwanza katika Jiji la Dar es Salaam, kwa mara ya kwanza tangu aanze kufanya kazi yake ya sanaa ya kuimba ambapo shoo hiyo itaitwa Kusnight na itaanza majira ya 12 jioni.

 

“Kwanza kabisa niwashuku­ru vyombo vya habari kwa sapoti yenu mnayotoa kwa kazi yetu lakini pia wito wenu mlioitikia kufika hapa, kikubwa zaidi WCB pamoja na Global Group tumeweza kushirikiana kuandaa shoo siku ya Idd Pili na tutaita Kusnight ambapo host wa shoo hiyo atakuwa Jackline Wolper na kwa nini tu­meita Kusnight? Unajua mimi ni mtu wa Kusini, nimezaliwa huko, nimesoma huko, huku Dar nimekuja kutafuta tu na wakazi wengi wa Mbagala ni watu wa Kusini, kwa hiyo hii ni nafasi kwao.

 

“Kwa nini Wolper? Una­jua hapa kati familia yangu ilikuwa na matatizo, hususan kwenye suala la mapenzi, wengi mnajua kuwa mpenzi wangu ni Sarah na watu wengi walijua kuwa walikuwa na bifu na Wolper, lakini sasa hawana bifu na washamaliza tofauti zao, tangia nianze ‘career’ yan­gu ya muziki sijawahi kufanya shoo katika mkoa wa Dar na hii ni nafasi yangu kuwafu­rahisha mashabiki wangu na Dar Live na mimi tuna historia kubwa sana, kwani kwa mara ya kwanza kukutana na Diamond, ilikuwa hapo, nikamueleza basi Diamond akamwambia yule DJ kabla hajapanda nianze mimi kwa shangwe nililopokewa, siku ile imenipa chachu ya kufanya shoo babkubwa siku hiyo ya Idd,” alisema Harmonize.

 

Naye meneja wa Dar Live, Rajab Mteta ‘KP’, alisema kuwa watakuwa na shoo kubwa siku ya Idd na kiin­gilio kitakuwa shilingi 10,000. Aliongeza kuwa wasanii wengi watakuwepo ila itakuwa ni sapraizi kwa mashabiki wa­takaojitokeza siku hiyo.

Comments are closed.