The House of Favourite Newspapers

Kwa Fabregas, Kila Kitu Kinawezekana

0
Cesc Fabregas

KESHO Jumapili, Chelsea itaikaribisha Manchester United katika Ligi Kuu England, kiungo wa timu hiyo Cesc Fabregas amesema timu yao itapambana kumaliza kileleni katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

 

Kauli hiyo ya Fabregas imekuja baada ya Jumanne wiki hii, Chelsea kufungwa mabao 3-0 na AS Roma katika mchezo wa Kundi C la ligi hiyo maarufu Ulaya.

 

Fabregas alisema: “Tunajua umuhimu wa kushiriki Ligi ya Mabingwa, mwaka uliopita tulikuwa na wiki nzima ya kufanya mazoezi na kuchukua mbinu za Conte (Kocha wa Chelsea, Antonio).

 

“Mwaka huu hatuna muda mrefu wa kujiandaa kwa sababu unacheza mechi Jumatano na Jumamosi, utafanya kitu gani Alhamisi pekee? Kukimbia? Haiwezekani.

“Unatakiwa kuwa fiti kwa wikiend  kumaliza kileleni katika Uefa, pia kufanya vizuri England katika ligi kuu.”

Chelsea inaikaribisha Man United kwenye Uwanja wa Stam-ford Bridge katika muen-delezo wa Premier League.

Leave A Reply