The House of Favourite Newspapers

Kwasi aanza hesabu za kimataifa

WAKATI Simba ikita­rajia kucheza mich­uano ya kimataifa mapema mwezi ujao dhidi Gendarmerie Tnale ya Djibouti, beki wa timu hiyo, Asante Kwasi ame­funguka kuwa wapo fiti na watapambana ingawa kwa sasa hakuna timu ya kud­harau.

Simba inatarajiwa kushiriki michuano hiyo baada ya miaka kadhaa kupita huku mara ya mwisho ikiwa ni msimu wa 2012/13 baada ya msimu wa nyuma yake kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara.

 

Beki huyo kwa sasa amekuwa chachu ya mafanikio licha ya ku­tua hivi karibuni ndani ya kikosi hicho am­bacho amekitumikia katika mechi mbili za ligi dhidi ya Singida na Kagera Sugar.

Kwasi alisema kuwa wanajipanga kupam­bana na upande wa kimataifa ni lazima wa­jitume kwa bidii hasa katika hatua ya awali ili kuweza kusonga mbele na kufanya vyema.

 

“Najua ni kazi ngu­mu lakini mechi hizi za kimataifa hakuna timu ya kudharau hata kidogo, sababu siku hizi kila timu inapigana kuhakikisha inapata matokeo mazuri na michuano ile ni lazima kufanya vizuri hasa sisi wachezaji kupata nafasi ya kujitangaza zaidi.

“Kwa upande wangu napam­bana kuhakikisha nashirikiana na wenzan­gu vyema ili kuweza kupata matokeo kwa me­chi zote ambazo tu­naende­lea ku­cheza ili kuwa vizuri,” alise­ma Kwasi.

Martha Mboma, Dar es Salaam

Comments are closed.