The House of Favourite Newspapers

Laptop ya Kwanza Duniani Yenye Skrini Tatu Yazinduliwa

laptop2Kampuni inayotayarisha michezo ya kompyuta ya Razer imezindua kompyuta mpakato (laptop) mpya ambayo yenye skrini tatu wenye maonyesho ya teknolojia mpya jijini Las Vegas, Marekani.

Kampuni hiyo imesema laptop hiyo ambayo imeundwa kupitia mradi uliopewa jina la Valerie, ndiyo ya kwanza ya aina yake duniani.

Skrini zote tatu zina ukubwa wa wa inchi 17 ( sawa na sentimita 43)  na uwezo wake ni pikseli 4,000 (4k), skrini mbili huchomoza kila upande kutoka kwa skrini kubwa ya kati, moja kwa moja. Sifa nyingine ni kuwa, kompyuta hiyo inapozimwa na kufungwa, inapungua upana wa inchi 1.5.

Mmoja wa wachanganuzi wa teknolojia mpya amesifu laptop hiyo na kusema wachezaji wa michezo ya kompyuta siku hizi wamekuwa wakitafuta kompyuta za kisasa zaidi, ghali na zenye uwezo wa kipekee.

laptop1

Razer wamesema inalingana na laptop nyingi zinazotumiwa kwenye michezo ya kompyuta, ambazo kawaida huwa kubwa kidogo kuliko kompyuta zinazotumiwa nyumbani na afisini.

laptop

Laptop iliyozinduliwa ni ya maonesho tu na Razer hawajasema ni lini wataanza kuunda kompyuta kama hizo za kuuza.

Project ya Valerie ni moja tu ya laptop za michezo ya kompyuta zilizozinduliwa kwenye maonesho ya CES.

Acer walizindua laptop kubwa ya inchi 21 ambayo inaitwa Predator 21X, ambayo inagharimu $8,999 (£7,250) ambazo ni sawa na TZS milioni 19.635.

Samsung nao wamezindua laptop yao ya kwanza ya michezo iitwayo Samsung Notebook Odyssey, ambazo ni za ukubwa mara mbili za inchi 15 na zingine za nchi 17.

Comments are closed.