The House of Favourite Newspapers

Lava Lava Ana Gundu WCB?

0

 

MEI 2017 msanii Lava Lava alianza kufyatua ngoma zake akiwa kwenye lebo kubwa ya muziki Bongo, WCB.

 

Nyimbo zake za Tuachane, Niuwe, Gundu, zilimfanya msanii huyo tukatukanwe kisela yaani asifiwe kiaina mitaani kwa kuambiwa: “Anajua hadi anaboa”.

 

Mwaka mmoja baadaye Mbosso akatia maguu WCB, akapiga Hodari, akafyatua Nadekezwa, akatoa Tamu basi akazidi kuwa mtamu pale Wasafi ambako msanii mkubwa Bongo Diamond ndiyo bosi wa lebo.

 

Aprili 2020, Zuchu naye aliingia anga za WCB kapiga zake, Nisamehe, akagonga Wana, akaachia Litawachoma, halafu akatoa Sukari na tangu hapo akawa ‘anayelambwa’ karibu kila mtaa.

 

Swali; kwa nini Lava Lava ameshindwa kutoboa kwenye gemu akiwa ndani ya WCB ingawa kipaji kikubwa anacho?

 

Wachache walimtania kwenye mitandao ya kijamii kuwa “huwezi kuimba Gundu” halafu ukategemea kupata bahati.

 

Ina maana Lava Lava ana Gundu WCB? Swali linakuwa gumu, ingawa kwa mbali unaweza kusema analo kweli, kutokana na nini ujue? Havumi kama wenzake.

 

Hata bosi wake Diamond amekuwa kando mno na yeye kwenye kufanya naye kolabo Unajiuliza kwa nini anamtenga msanii huyo tofauti na Mbosso na Zuchu ambao ameshirikiana nao kwenye tungo kibao?

 

Bila shaka kuna siri nzito katika jambo hili, mfumbua siri hiyo anabaki kuwa Lava Lava pengine siku zikitimia atakuja kusema jambo lililo nyuma ya pazia katika safari yake ya muziki.

 

Ila kusema kweli msanii huyo hapaswi kuchukuliwa poa, kwani ngoma zake zimekuwa zikifanya vizuri, kwani hata hii mpya ya Nikomeshe inakimbiza mjini YouTube, ingawa siyo kwa kasi kubwa.

 

Leave A Reply