Lava Lava Atikisa Na Ndinga La Kifahari!

DAR ES SALAAM: Ukiwa umekatika mwaka mmoja na miezi kadhaa tangu atambulishwe rasmi kama memba wa Kundi la Wasafi Classic Baby (WCB), msanii wa Bongo Fleva, Abdul Juma Idd ‘Lava Lava’ ametikisa baada ya kununua ndinga la kifahari aina ya Toyota Soarer (Open Roof).  Lava Lava alijiunga na lebo hiyo mwaka 2017 na kuachia kwa mara ya kwanza wimbo wake wa Tuachane na tangu hapo hakuwahi kuonekana akiwa na ndinga la kifahari.

Juzikati kupitia ukurasa wake wa Instagram, mkali huyo anayetikisa na Wimbo wa Habibi alianika ndinga hilo jipya linalokadiriwa kuwa na thamani kuanzia Dola za Kimarekani 19,000 (zaidi ya shilingi milioni 43 za Kitanzania) na kuwapongeza viongozi wake wote wa WCB waliomsaidia pamoja na mashabiki wake wote walioonesha sapoti kuanzia ameanza muziki wake hadi alipofikia.

“Tangu nilipoanza mpaka sasa nilipofikia kijana wenu nimeongeza kausafiri na hii si kwa sababu ni tajiri sana, hii ni kwa sababu ya sapoti yenu tangu mwanzo wa safari yangu ya muziki.

“Ewe kijana mwenzangu dada, kaka na wote wahangaikaji tusikate tamaa Mungu yupo anatuona tusali na tufanye kazi kwa bidii, nakumbuka miaka mitatu nyuma nilikuwa sina uwezo wa kununua hata baiskeli ila maombi juhudi na kumuheshimu kila mtu ndiyo nguzo ya mafanikio, tusikate tamaa Mungu anatuona.”

Mara baada ya kutupia mitandaoni picha akiwa amezungukwa na baadhi ya wasanii wenzake huku kwenye posti hiyo kila mmoja akimsifia kwa ndinga hilo, Gazeti la Ijumaa lilimtafuta Lava Lava kujua undani wa ndinga hilo ambapo alikiri ni lake wala siyo maigizo.

Ijumaa: Nikupe hongera kwa kununua gari, unaweza kutuambia ni lako kweli au unauzia sura tu?

Lava Lava: Kuna watu wengine ni ngumu kuamini kama kweli naweza kuvuta gari kama hili, lakini niwahakikishie kweli gari ni langu.

Ijumaa: Lakini inadaiwa kuna mkono wa muigizaji Irene Uwoya ambaye anaonekana kama ni mwandani wako wa sasa?

Lava Lava: Kwa hiyo ina maana mimi siwezi kununua? Sikiliza niwaambie, si kwamba Uwoya hana uwezo wa kumnunulia mtu gari, anao sana tu na anaweza kumnunulia mtu yeyote yule.

Hao wanaosema ameninunulia huenda walisikia anataka kuninunulia, kwa hiyo hilo analotaka kuninunulia likinifikia nitashukuru

Stori: Neema Adrianl, Ijumaa


Loading...

Toa comment