The House of Favourite Newspapers

Lava Lava Avunja Ukimya Kusepa Wasafi

0

SITOJIFANYA maproso…Nikaja kukudanganya…Ukakumbuka before…N’takupenda mpaka useme poo…Kwako nitang’ang’ana I’ll never let you go…Mtegoni nimenasa ka tandabui kwa ukuta…Believe me I don’t lie (I don’t lie)…Nishaacha anasa nimeweka nukta…I’m ready to fly (I’m ready to fly with you baby)…Yeah mengi yatasemwa kwamba mimi ni player…

 

Wanapenda tukigombana…Eti nakuchezea…Roho zawauma tumebaki kidedea…Twende tukiongozana…Wawili kama pair…Vunja kabati…Vunja kabati…Vaa pendeza nogesha tutoke…Baby vunja kabati oh…

 

Komesha komesha (Aristotee)…Fanya unajipinda pinda kata…Mugongo pinda pinda kata…Fanya unajipinda pinda kata…Mugongo pinda pinda kata…”
H
II ni sehemu ya mashairi matamu ya Ngoma ya Komesha kutoka kwa mzee wa malavidavi kunako Bongo Fleva, Mr Love Bite au Lava Lava.


Majina yake halisi
yanasomeka Abdul Iddi kwenye Kitambulisho cha Taifa (NIDA), leseni ya udereva na kwenye vitambulisho vingine.

 

Ni kichwa kingine ambacho ni prodakti ya Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) ya mtu mzima Nasibu Abdul au Diamond Platnumz.

 

Pale WCB, Lava Lava yupo na wakali wengine kama Rayvanny, Mbosso Khan, Queen Darleen na kitinda mimba wao, Zuchu.

 

Lava Lava ni miongoni mwa vijana wanaofanya vyema kunako Bongo Fleva kwa sasa. Alijiunga na Wasafi mwaka 2015, lakini alikuja kutambulishwa rasmi siku ile ya Mei 22, 2017.

 

Safari ya muziki ya Lava Lava haikuwa rahisi kama baadhi ya watu wanavyodhani kwani mwenyewe anasema ilianzia mtaani kwao, Bunju jijini Dar es Salaam.

 

Alijenga jina kwa kuimba nyimbo za wasanii wengine wakubwa wa ndani na nje ya Bongo, kiasi kwamba asipokuwepo mtaani hapo, pengo lake huonekana.

 

Lava Lava alitoroka shule na kwenda Nyumba ya Kukuza Vipaji (THT) kwa ajili ya kuimba baada ya kupita kwenye mchujo wa wasanii wachanga zaidi ya 1,000 na kuingia kwenye 50 bora.Lava Lava alifanya mafunzo ya muziki ndani ya THT kwa miaka mitano na kukabidhiwa cheti cha ufuzu masuala ya muziki na kupewa ruhusa ya kuingia mtaani kusaka au kutafuta menejimenti.

 

Mwamba Lava Lava ameweka rekodi na ngoma kali kama Go Gaga, Walewale, Utatulia, Tuachane, Gundu, Yalah, Najidai na nyingine kibao ambazo ziliteka na zinateka vichwa vya mashabiki wake ndani na nje ya Bongo.

 

Hata hivyo, Lava Lava amekuwa akipita kwenye mjadala mkali kwamba, huwenda haendani au anazidiwa na ukubwa wa Wasafi hivyo kushindwa kufurukuta kiasi cha kupitwa hadi na Zuchu ambaye ana mwaka mmoja na miezi minne tu kwenye muziki, lakini amefanya makubwa na kuweka rekodi za aina yake.

 

Wapo baadhi ya mashabiki wake wamekuwa wakidai kwamba, hawamuelewi kabisa kwani amepoa ukilinganisha na vichwa vingine ndani ya Wasafi ambao ni mabingwa wa kutrendi kwenye mitandao ya kijamii na kujikusanyia mamilioni ya watazamaji (views) wa kazi zao.

 

Wapo pia wanaodai kuwa, huwenda yupo mbioni kusepa kwenye lebo hiyo baada ya kuona mambo hayajipi kama alivyotarajia.

 

Katikati ya mjadala huo, IJUMAA SHOWBIZ imemtafuta Lava Lava na kufanya naye mahojiano maalum (exclusive interview) ili kujua mawili matatu kuhusiana na hayo yanayosemwa na tetesi kwamba yupo mbioni kuachana na Wasafi;

IJUMAA SHOWBIZ: Mambo vipi Mr Love Bite?

LAVA LAVA: Salama kabisa, Mwenyezi Mungu anajaalia uzima upo.

IJUMAA SHOWBIZ: Lava Lava leo nimekutafuta ili tuweze kuzungumza juu ya ukimya wako, watu wanasema huwiki kama zamani, tatizo ni nini, ukitoa ngoma hadi inasahaulika?

 

LAVA LAVA: Inasahaulika kivipi? Mbona nimeachia ngoma juzijuzi tu hapa? Haina hata muda mrefu, nimeachia ngoma nikiwa na Mbosso, inakwenda kwa jina la Basi Tu!

 

IJUMAA SHOWBIZ: Mashabiki wanatamani kuona ukifanya kazi nyingi kama zamani ndiyo maana wanakuwa na wasiwasi…

 

LAVA LAVA: Mbona nafanya? Wanataka nifanyeje?IJUMAA SHOWBIZ: Wanataka kuona ukifanya ngoma back to back kama zamani…

 

LAVA LAVA: Sawa, nimewaelewa mashabiki wangu hivyo nitakuwa nafanya kama wanavyotaka ila wanatakiwa kujua kwamba muziki unatakiwa kusoma soko kwanza linakwendaje.

 

IJUMAA SHOWBIZ: Lava Lava pamoja na kusoma soko ila kwako usomaji wako hadi unapotea, watu wanatamani kuona manjonjo yako…

 

LAVA LAVA: Sawa nimewaelewa mashabiki wangu wanataka kitu gani.

 

IJUMAA SHOWBIZ: Au wewe unahisi Lava Lava au Mr Love Bite wa sasa hivi ni kama yule wa zamani kweli?

LAVA LAVA: (mmmmh) kiukweli mimi najiona nipo vilevile tu kama zamani.

 

IJUMAA SHOWBIZ: Au ndiyo tuseme kufanya kazi na bosi mkubwa kama Diamond hufi na njaa maana hata usipoimba, utakula, utavaa na utaendesha ndinga kali kila siku?

 

LAVA LAVA: Hapana, siyo kweli kufanya kazi na Big (Diamond) hakunifanyi mimi kubweteka, mbona nafanya?

 

IJUMAA SHOWBIZ: Na vipi kuhusiana na hizi tetesi kwamba unataka kusepa au kuacha kufanya kazi na Wasafi zimekaaje?

 

LAVA LAVA: Taarifa hizo hazina ukweli wowote. Mimi nipo kwenye familia ya Wasafi mwanzo hadi mwisho.

 

IJUMAA SHOWBIZ: Na utawathibitishiaje mashabiki wako kwamba utadumu Wasafi maana kuna vitu wanaviona wanadai kwamba hawavielewi?

 

LAVA LAVA: Vitu kama vipi ambavyo hawavielewi?

 

IJUMAA SHOWBIZ:
Umepoa sana siyo
kama zamani; yaani upo kama umejitenga na wenzako, hii imekaaje?

LAVA LAVA: Mimi ndani ya Wasafi bado nipo sana, wala sijawaza wala kufikiria kuondoka.

IJUMAA SHOWBIZ:
Ahsante kwa ushirikiano wako.

 

Leave A Reply