The House of Favourite Newspapers

Leo Ndiyo Leo Jahazi Dar Live

0

8&9risasi copyMzee Yusuf

Na Mwandishi Wetu

HATIMAYE! Ile siku iliyokuwa ikisubiriwa na wapenzi wa burudani imewadia ambapo kundi lisilo na mpinzani kunako Muziki wa Taarab, Jahazi Modern linatarajiwa kuitambulisha rasmi albamu yao ya Kaning’ang’ania leo, Machi 12 ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar.

Akizungumza na Risasi, Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo alisema kuwa pazia la burudani litafunguliwa kuanzia saa mbili usiku na kuahidi kuwa kutakuwa pia na ‘red carpet’ hivyo mashabiki wajitokeze kwa wingi.

“Usiku wa leo utakuwa wa bandika bandua kwani Jahazi wakiongozwa na Mzee Yusuf, watapiga nyimbo zao zote kali kuanzia Chozi la Mama, Mahaba Niue sambamba na kuizindua Albamu ya Kaning’angania,” alisema Mbizo na kumalizia kuwa kiingilio kitakuwa ni 8,000 tu getini.

Leave A Reply