LEYLA ALIYEUAWA UINGEREZA AZIKWA KWAO ARUSHA (Picha + Video)
MKUU wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, jana ameongoza mamia ya waombolezaji katika maziko ya marehemu Leyla Mtumwa aliyeuawa na mumewe, Kema Kasambula, kwa kuchomwa visu mwezi uliopita jijini London nchini Uingereza.Mazishi hayo yamefanyika katika makaburi ya Sinoni jijini Arusha.
Mwili wa Leyla uliokuwa ukishikiliwa na Jeshi la Polisi nchini Uingereza kwa ajili ya uchunguzi ulikabidhiwa kwa familia yake na kuletea nchini Jumatatu.
Leyla anadaiwa kuuawa na mumewe huyo, usiku wa kuamkia Machi 30, mwaka huu jijini humo na sasa anakabiliwa na kesi ya mauaji.
(Habari na Korumba Moshi, Arusha)
Comments are closed.