The House of Favourite Newspapers

Libya Yaunda Serikali ya Mpito

0

WAJUMBE wa pande hasimu kisiasa nchini Libya jana Februari 5, 2021, wamefanikiwa kumchagua waziri mkuu na wajumbe watatu wa baraza la urais, ambao wataiongoza serikali ya mpito ya kitaifa kuelekea uchaguzi mkuu mwishoni utakofanyika Desemba mwaka huu.

 

Mkutano wa wajumbe hao 74 umemchagua na balozi wa zamani wa Libya nchini Ugiriki, Mohammed Menfi, kuongoza baraza la urais na  mfanyabiashara, Abdul-Hamid Mohammed Dbeibeh, kuwa waziri mkuu

 

Kuchaguliwa kwa serikali ya pamoja ya mpito kuna lengo la kumaliza mgawanyiko nchini Libya, ambapo kwa miaka mitano iliyopita nchi hiyo ilikuwa na serikali mbili; moja yenye makao mjini Tripoli ikiongoza upande wa magharibi, huku nyingine iliyoungwa mkono na makundi kadhaa yenye silaha ikiidhibiti sehemu ya mashariki ya nchi hiyo.

 

Mkutano huo umesimamiwa na Umoja wa Mataifa.  Tangu kuuwawa kwa kiongozi wa taifa hilo, Muammar  al-Gaddafi, Octoba 2011, nchi hiyo iliingia kwenye machafuko ya vita ya wenyewe kwa wenyewe na kusababisha vifo vya maelfu ya raia wasiokuwa na hatia.

Leave A Reply