The House of Favourite Newspapers

Licha ya Simb kupoteza Dhidi ya Horoya …Manula Shujaa, Apangua Penalti Kiufundi

0

SIMBA ilishindwa kutamba ugenini katika mchezo wake wa kwanza wa Hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Horoya, huku kipa wake Aishi Manula akiibuka shujaa katika mchezo huo.

Horoya walifanikiwa kuondoka na ushindi wa bao 1-0. Bao la wapinzani wa Simba lilifungwa na Pape Ndiaye dakika ya 18 ya mchezo huo.

Mchezo huo ulikuwa na matumizi makubwa ya nguvu ndani ya Uwanja wa General Lansana Conte ukiwa ni mchezo wao wa kwa timu hizo za Kundi C.

Licha ya Simba kupoteza, Manula aliibuka kuwa shujaa baada ya kupangua penalti ya wapinzani wao dakika ya 71 mpigaji akiwa ni Ndiaye japo kabla ya hapo alikuwa ameokoa hatari mara kadhaa katika dakika tofauti 4, 8,13,14 na 40 za kipindi cha kwanza.

Simba walimalizwa na wapinzani  kutokana na kutumia mipira  ya juu zaidi na wengi wao ni warefu hata bao lilipatikana kwa kichwa kupitia mpira wa kona.

Hata hivyo,umakini hafifu kwa safu ya ushambuliaji wa Simba ambapo nahodha John Bocco alikosa nafasi mbili ikiwa ni pamoja na ile ya wazi akiwa na kipa dakika ya 79.

Baada ya hapo, Simba watavaana na Raja Casablanca Uwanja wa Mkapa, Dar es Saalam Februari 18, mwaka huu mchezo wa pili hatua ya makundi.

MWANDISHI WETU, SPOTI XTRA, JUMAPILI

KIJANA AUAWA KWA KUSUKUMWA GHOROFANI DAR, SUNGUSUNGU WATAJWA KUHUSIKA- ”KICHWA CHOTE KIMEHARIBIKA”


 

Leave A Reply