The House of Favourite Newspapers

Lifti Yakatika Kutoka Ghorofa Ya 10, Saba Wajeruhiwa, Kamanda Azungumza -Video

0

Lifti katika jengo la LAPF Millenium Tower lililopo Makumbusho jijini Dar es Salaam, imeporomoka ikiwa na watu ndani na kusababisha majeruhi kadhaa.

Mkaguzi Msaidizi wa jeshi la Zimamoto na Uokoaji Patrick Afande amesema, chanzo cha lifti hiyo kuporomoka ni kuzidisha idadi ya watu tofauti na uwezo wake ambapo wakati tukio hilo linatokea ilibeba zaidi ya watu 10.

Lifti hiyo imeporomoka kutoka ghorofa ya 10 na kujeruhi watu 7 ambao wamepelekwa katika hospitali ya Kairuki, Dar es Salaam kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Leave A Reply