The House of Favourite Newspapers

LIN BARBECUE & COLLECTION WAUNGANISHA WASANII KUSAIDIA YATIMA

Watoto wakionesha kipaji chao cha kuimba, wengine ni viongozi wa kituo hicho.

Wasanii wa filamu na muziki jana wameungana na uongozi wa Kampuni ya Lin Barbecue na Collection kupigania maisha ya watoto yatima wa kituo cha Yogo kilichopo Mbezi jijini Dar.

Matukio kaika Picha:

Chuchu Hans (kushoto) akikabidhi msaada kwa moja wa viongozi wa kituo hicho.

Kampuni ya Lin Barbecue ambayo jana ilizindua mgahawa wa kisasa na duka la mavazi eneo la Sinza Africasana jijini Dar ni walezi wa kituo hicho.

Mkurugenzi wa Lin Barbecue, Newton Mwakifamba (kushoto) akimkabidhi vifaa mmoja wa watoto

Katika hafla hiyo, wasanii mbalimbali walijitokeza na kuahidi kuwasaidia watoto hao. Miongoni mwao ni Hemed Suleiman ‘PHD’ Yusuph Mlela, Chuchu Hans, Hassan Mussa ‘Super Nyamwela’ Peter Msechu’ Amini Mwinyimkuu, Tausi Mdegela, Rommy Jones na wengine.

Hemed Suleiman (kushoto) na Yusuph Mlela wakiwa eneo la tukio.

Mwanamuziki Amini (kushoto) na Peter Msechu (kulia) wakiwa na wakurugenzi wa Lin Barbecue na Lin Collection.

Yusuph Mlela akiwa kwenye Bufee la Lin Barbecue.

PICHA: RICHARD BUKOS / GPL

Comments are closed.