The House of Favourite Newspapers

Mkude, Wawa Wamvuruga Kagere

 

Jonas Mkude

WACHEZAJI wa Simba, Jonas Mkude na Pascal Wawa juzi walionekana wakimvuruga mshambuliaji wa timu hiyo, Meddie Kagere wakati wa mazoezi.

 

Simba ilifanya mazoezi juzi kwenye Uwanja wa Boko Veterani jijini Dar wakijiandaa na mchezo wa kesho wa ligi kuu dhidi ya Stand United.

 

Katika mazoezi hayo yaliyosimamiwa na kocha mkuu, Mbelgiji, Patrick Aussems, alionekana akiwakazania wachezaji wake Kagere, Said Ndemla, Shiza Kichuya na Shomary Kapombe kufunga kwa kutumia mipira ya faulo sasa hapo ndipo palizua jambo.

Wakati mazoezi yakiendelea, Wawa ambaye ni raia wa Ivory Coast na Mkude walikuwa wametulia pembeni wakiangalia mazoezi hayo ndipo wakaona Kagere akishindwa kufanya kile ambacho kocha alikuwa akikihitaji.

 

Baada ya kuona hivyo walianza kumvuruga kwa kumuonyesha kwa ishara kwamba akapumzike kwani.

Comments are closed.