The House of Favourite Newspapers

LINA: NITAZAA WATOTO 3 TU

Picha inayohusiana

STAA wa Filamu za Kibongo, Esterlina Sanga, ameibuka na kusema ataongeza mtoto wa pili miaka miwili ijayo kwani mpango wake ni kuwa na watoto watatu katika familia yake. Akiongea na Risasi Jumamosi, Linah alisema kuwa, atazaa watoto watatu kwani ndiyo anaotamani kuwa nao na kwamba baada ya mtoto wake aitwaye Paris kufikisha miaka miwili ‘atafyatua’ mwingine.

Linah ambaye ameachia wimbo wake wa ‘Nikoleze’ juzi kati na kuachia picha matata mtandaoni iliyowatoa udenda baadhi ya wanaume wakware, alieleza kuwa anapenda sana watoto hivyo mmoja hatoshi. “Maisha bila watoto ni magumu, pamoja na kazi yangu ya muziki ninahitaji kuwa mama bora, hivyo nitazaa kama wanawake wengine,” alisema Linah ambaye ameomba mashabiki wake wapokee vema nyimbo yake kwani si ya kuikosa.

Na: Mwandishi Wetu

Comments are closed.