The House of Favourite Newspapers

Linah Shayo Wa Kigamboni Aibuka Na Milioni 5 Ya Magifti Dabo dabo Ya Tigo Wiki Hii

0
Meneja wa Tigo Kanda ya Temeke na Kigamboni, Jensen Msechu (kulia) akimkabidhi mfano wa hundi mshindi Linah Shayo.

Dar es Salaam, 18 Januari 2024: Mkazi wa Kigamboni jijini Dar, Linah Shayo, leo amekabidhiwa pesa shilingi milioni 5 alizojishindia katika kampeni ya Majifti Dabo dabo inayoendeshwa na kampuni ya mtandao wa simu za mkononi ya Tigo kwa wateja wanaotumia huduma mbalimbali za kampuni hiyo.

Linah Shayo akishangilia ushindi wake na mfano wa hundi ya pesa aliyojishindia.

Akizungumza wakati wa kumkabidhi mfano wa hundi ya fedha alizojishindia mshindi huyo (Linah)  Meneja wa Tigo Kanda ya Temeke na Kigamboni, Jensen Msechu amewataka watumiaji wa simu za mkononi kutumia mtandao wa Tigo kwa huduma mbalimbali kama vile kununua bando kwa kutumia Tigo Pesa au vocha za kukwangua, kununua muda wa maongezi, kulipa bili kutumia lipa namba kufanya manunuzi, malipo ya kiserikali na huduma nyinginezo.

Msechu amesema kwa kufanya hivyo nawe unaweza kuibuka mshindi kama ilivyokuwa kwa mshindi huyo alivyojiondokea na bahati hiyo bila kutarajia.

Mshindi Linah Shayo akishangilia ushindi wake pamoja na wafanyakazi wa Tigo.

Msechu amesema kampeni hiyo bado inaendelea ambapo wateja wa Tigo nchi nzima wataendelea kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo pesa taslimu shilingi milioni moja, milioni tano na milioni 30 katika droo ya mwisho. Sambamba na pesa taslimu kuna zawadi ya seti ya vifaa vya nyumbani vya kisasa kutoka Kampuni ya Hisense ikiwemo Tv, microwave, friji na seti ya muziki (sound bar). Alimaliza kusema Meneja Msechu.

Kwa upande wake mshindi huyo amesema awali ushindi huo kwake aliona kama ndoto lakini kitendo cha kukabidhi wa fedha hizo kupitia simu yake ya mkononi ndiyo kilichomdhihirishia us hindi wake. Linah amewashauri watumiaji wengine wa simu za mkononi kutumia mtandao huo ili nao wajaribu bahati zao.

Leave A Reply