The House of Favourite Newspapers

LIPULI WASAKA POINTI 10

BENCHI la ufundi la Klabu ya Lipuli FC ya Iringa limefunguka kuwa kwa sasa linajipanga kuhakikisha linavuna pointi 10 kwenye michezo yao minne ijayo yenye dakika 360, ambazo zitawapa uhakika wa kubakia kwenye Ligi Kuu Bara kwa msimu ujao.

 

Kwa sasa Lipuli FC iliyopanda daraja msimu huu, inashika nafasi ya saba kwenye msi­mamo wa ligi kuu ikiwa na pointi 30 baada ya michezo 18 iliyoshuka dimbani hadi sasa. Mara ya mwisho walicheza na Azam na ku­toka suluhu katika Dimba la Samora mkoani Iringa.

 

Kocha Msaidizi wa Lipuli, Selemani Mato­la, ameliambia Championi Jumatano kuwa, wameweka malengo hayo ya kupata pointi 10 kwenye mechi 11 zilizobaki kwa kuwa ili timu ibakie kwenye ligi inatakiwa kuwa na pointi 30 na kuendelea.

 

“Kama unavyoona kwa sasa tuko nafasi ya saba kwenye ligi tukiwa na pointi 20 lakini tulipo tunapiga mahesabu ya kukusanya pointi 10 ili tufikishe 30 ambazo zitatuweka mbali na mstari wa kushuka daraja na kuen­delea kuwepo kwenye ligi kwa msimu ujao,” alisema Matola.

 

Said Ally, Dar es Salaam

Comments are closed.