The House of Favourite Newspapers

LIPUMBA Amvaa Maalim Seif “Kesi 30, Anaongea na Sumaye” – VIDEO

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba amelaani vitendo vya Katibu Mkuu wa Chama hicho, Maalim Seif, vya kufungua na kuendeleza kesi mahakamani.

 

Akizungumza na waandishi mapema leo, Prof Lipumba amesema mpaka sasa Maalim Seif ameshafungua kesi zisizopungua 30 ambapo amedai lengo lake hasa ni kuweza kukihujumu chama na kukidhoofisha kabisa.

 

Aidha Prof Lipumba amewashukuru mawakili wao kwa juhudi kubwa wanazozifanya ambapo mpaka sasa wamefanikiwa kupangua na kushinda kesi 12 na kutoa wito kwao waendelee kupambana na kuhakikisha wanashinda kesi zote.

VIDEO: MSIKIE LIPUMBA AKIFUNGUKA

Comments are closed.