The House of Favourite Newspapers
gunners X

Lissu, Heche na Naibu Katibu Kuripoti Makao Makuu Mikocheni Kesho

0
Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, (Chadema) Tundu Lissu

Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, (Chadema) Tundu Lissu anatarajiwa kuripoti makao makuu ya chama hicho Mikocheni jijini Dar es Salaam kesho na kuanza kazi rasmi.

Taarifa iliyotolewa na idara ya mawasiliano, itikadi na mambo ya nje ya Chadema imesema Lissu atafuatana na Makamu Mwenyekiti (Taifa) wa Chadema, John Heche. Aidha katika msafara wao atakuwepo pia Naibu Katibu Mkuu Bara wa Chadema, Amani Golugwa.

Taarifa hiyo imesema Lissu na ujumbe wake utapokelewa na Katibu Mkuu John John Mnyika ambaye atawatambulisha watendaji wa makao makuu ya chama hicho.

“Chama kinawakaribisha viongozi wa chama kutoka Zanzibar, viongozi wa Kanda ya Pwani na viogozi wengine na wanachama ili waweze kumpokea mwenyekiti wa chama hapa makao makuu ya chama,” imesema taarifa hiyo.
Lissu alichaguliwa na Mkutano Mkuu wa Chadema Januari 21 mwaka huu katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, alimshinda Freeman Mbowe ambaye alihudumu katika nafasi hiyo kwa miaka 21

RAIS wa BENKI ya DUNIA AUWASHA MOTO MBELE ya RAIS SAMIA – MJADALA wa MOTO MATUMIZI ya NISHATI….


 

Leave A Reply