The House of Favourite Newspapers

Lissu: Utafiti Ulionyesha Lowassa Alibeba 18% ya Kura Zote

lissu-global-tv-4  Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu katika kitabu cha wageni alipowasili kwenye Ofisi za Global Publishers kwa mahojiano leo.lissu-global-tv-6

Tundu Lissu akijibu swali la mwandishi wa habari wakati wa mahojiano hayo.

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema kiliamua kumchukua aliyekuwa waziri mkuu, Edward Lowassa, ajiunge na chama hicho baada ya kubaini katika utafiti maalum uliofanywa na shirika moja kutoka nchi za nje kwamba alikuwa na uwezo wa kubeba asilimia 18 ya kura zote katika uchaguzi mkuu kuliko mgombea mwingine wa urais katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka jana huku aliyekuwa akimfatia akiwa na asilimia 12 pekee.

lissu-global-tv-8Tundu Lissu akifafanua jambo.

Hayo yalisemwa na Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu, wakati akihojiwa na Global TV Online leo ambapo alisema pamoja na Lowassa kuongoza wagombea wote katika utafiti huo, suala la ufisadi lililokuwa linadaiwa kumhusu,  halikuwa kipaumbele cha mamilioni ya wapiga kura nchini.

lissu-global-tv-11Lissu akiwa na Mhariri wa Gazeti la Uwazi, Elvan Stambuli

Alifafanua kwamba suala la ufisadi lilikuwa katika nafasi ya tano katika vipaumbele vya wapiga kura, likiwa limetanguliwa na mambo muhimu  kama vile mahitaji ya maji safi na salama, usafiri bora, huduma bora za afya na mahitaji  mbalimbali ya kuwawezesha wananchi kiuchumi.

lissu-global-tv-15Lissu akiwa na viongozi mbalimbali wa Global Publishers.

Utafiti huo, alisema ulikuwa msingi wa kumchukua mwanasiasa huyo katika chama hicho, ikiwa ni pamoja na kanuni ya maisha na kisiasa kwamba binadamu hawezi kuwa na marafiki au maadui wa kudumu.

NA WALUSANGA NDAKI/GPL

Polisi Wakabiliana Vikali na Majambazi Mikocheni

Comments are closed.