The House of Favourite Newspapers

KUTOKA BUNGENI: Mkutano wa Bunge – Maswali na Majibu (Aprili 23, 2018)

Mbunge Kassim Ally ameululiza Serikali ina mpango gani kuifanya TANESCO ijiendeshe kwa faida ambapo Naibu Waziri wa Nishati, amemjibu Serikali inaongeza uwekezaji katika mitambo ya kufua umeme kwa gesi na maji kuepukana na mitambo ya mafuta kupunguza gharama za uendeshaji kwa TANESCO.

 

Aidha, amesema TANESCO inakabiliwa na gharama kubwa za uendeshaji na mapato ya shirika hayakidhi. Pia amesema, shirika linakabiliwa na malimbikizo ya madeni kwa wateja. Serikali inaendelea na mpango wa Stiegler’s utakaozalisha umeme nafuu.

 

Mbunge Halima Bulembo amesema hasara ya TANESCO imekuwa ikiongezeka kwa Kasi kati ya 2015-17 ambapo Waziri wa Nishati, dkt. Medard Kalemani ameeleza uzalishaji wa umeme umeongezeka kuliko miaka ya nyuma pia mapato ya TANESCO yameongezeka maradufu kutoka bilioni 29.1 mpaka 32.3.

 

Comments are closed.