The House of Favourite Newspapers

UKAWA Watishia Kususia Uchaguzi wa Januari 13, Endapo Serikali Haitafuata Haya (Video)

VIONGOZI wa Vyama vya Upinzania Vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) wamekutana na kufanya mazungumzo na wanahabri leo Jumatatu, Desemba 11, 2017 Hotel ya Colosseum Hotel, Oysterbay, jijini Dar es Salaam ambapo wamefunguka mengi ikiwemo hali ya kisiasa hapa nchini kwa sasa na tathmini ya uchaguzi uliofanyika hivi karibuni.

Katika mkutano huo uliokuwa na lengo la kujadili hali ya kisiasa nchini, Mwenyekiti wa CHADEMA, Mh. Freeman Mbowe asema kwa yanayoendelea nchini ni dhahiri kuwa demokrasia imekiukwa.

“Tumejadili tumeona hakuna haja ya sisi kama Taifa kufanya uchaguzi wa Januari 13, 2018 uliotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) hivi karibuni, badala yake uchaguzi usogezwe mbele. Vyama vya siasa na wadau wahusishwe ili waweze kutafakari. Tukubaliane kuhusu maadili ili yasikiukwe.

“Uchaguzi huu uahirishwe ili wahusika wakatafakari kuhusu tulikotoka, tulipo na tunakotaka kwenda. Kama Tume na Serikali watapuuza, Rai Yetu, basi sisi kama UKAWA hatutakuwa tayari kushiriki uchaguzi huo wa januari 13, 2018 hatutashiriki,” alisema Freeman Mbowe.

Mbowe ameongeza pia kuwa, Uchaguzi Mdogo uliofanyika siku za hivi karibuni ulikuwa kama vita hasa kwa Vyama vya Upinzani. 

“Uchaguzi mdogo uliofanyika hivi karibuni ulikuwa kama vita, hasa kwa vyama vya upinzani, kwani tumeona umwagaji wa damu katika uchaguzi huo. Wakati hayo yote yakitokea Jeshi la Polisi walikuwa kiangalia.

“Upinzani tulizuiwa kufanya kampeni / siasa eti kwamba ni wakati wa kujenga nchi, lakini tunaona Chama Cha CCM wanafanya mikutano ya hadhara. Kazi ya Jeshi la Polisi ni kulinda raia bila kushurutishwa na mtu, tunashangaa Jeshi letu la Polisi limekua la CCM.

“Matukio kama haya ya kuminya na kugandamiza demokrasia katika uchaguzi yakiendelea, mjue hakuna tena uchaguzi wowote utakaofuata sheria ya nchi.” alisema Freeman Mbowe.

Kwa upande wake kiongozi wa CUF, Julius Mtatiro amesema suala la vyama vya upinzani kutoa matamko kwa serikali halafu hakuna kinachotekelezwa, wao kama upinzani hawatajachoka, watapambana hadi kieleweke.

Comments are closed.