The House of Favourite Newspapers

The LiFe Club ‘Maisha Basement’ Kuzinduliwa Usiku wa Leo Ijumaa Dar

Meneja wa burudani wa klabu  ya The Life Club, Hemed Kavu ‘HK’.

Klabu maarufu ya burudani ya The Life Club  ‘Maisha Basement’ leo Ijumaa usiku inazinduliwa upya kwenye makao yake mapya yaliyohamishiwa katika ukumbi Mwenge Old Cinemax Century jijini Dar es Salaam. Zamani Klabu hiyo ilikuwa na maskani yake Makumbusho katika jengo la Milenium Tower.

 

Meneja wa Burudani wa The Life Club, Hemed Kavu ‘HK’ ameiambia  Global TV Online leo Ijumaa kuwa  wamejiandaa kutoa burudani ya aina yake na  katika uzinduzi huo  wamealikwa mastaa mbalimbali wa Bongo Fleva na wasanii wa muvi. Kiingilio kitakuwa Tsh 10,000/- kawaida na 20,000/- kwa VIP.

 

Uzinduzi huo unaanza saa tatu usiku amewaomba wapenda burudani kufika Mwenge Old Cinemax Century kujionea Klabu namba moja Tanzania kwa ubora wa kila kitu.

 

Pia ameongeza kuwa watakuwa wanatoa burudani kuanzia siku ya  Jumanne mpaka Jumapili na wameweka mambo mengi ya kisasa ambayo mashabiki hawatajutia.

Comments are closed.